Inaweza kuwa ni ngumu sana kwako kufanya mazoezi ila zoezi la kuruka kamba lina faida nyingi sana ikiwemo hizi hapa:-

Kamba ya kuruka kwa muda mrefu imekuwa ikitumiwa na wanamazoezi kama vile mabondia lakini pia ukiruka kamba inasaidia kuongezeka kwa kiwango cha moyo na kupumua sawa na ukiruka kwa dakika kumi kila siku, utaona mabadiliko kwenye mwili wako.
Kuruka ni mazoezi kamili ya mwili ambayo hutumia misuli yako ya tumbo, miguu na mabega pamoja na mikono hivyo husaidia kukaza kama inakuwa imelegea.
Pia kuruka kamba huongeza madini kwenye mfupa hivyo unashauriwa kuruka japo mara tatu kwa wiki.