Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dk Albina Chuwa amesema Juhudi za Serikali katika kuendelea kuimarisha sekta ya afya zimezaaa matunda ambayo ni kuongeza wastani wa umri wa kuishi kwa Watanzania.
Dk Chuwa ameyasema hayo Oktoba 28, 2023 katika Uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto na viashiria vya Malaria Tanzania ya mwaka 2022 iliyofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam na kuongeza
Dk Chuwa amesema miaka ya nyuma wastani wa kuishi wa Watanzania ilikuwa ni miaka michache akisema mwaka 1978 wastani wa umri wa kuishi wa Watanzania ulikuwa ni miaka 44 lakini kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2022 takwimu zinaonesha kuwa wastani huo umeongezeka na kufikia asilimia 65.5.