UMEME WABISHA HODI VITONGOJI 60 IKUNGI MASHARIKI, MGONTO ATOA ‘RAMANI’

Na Saulo Stephen – Singida.

Jumla ya Vitongoji 60, Vilivyopo katika Jimbo la Ikungi Mashariki Mkoani Singida vinatarajia kuunganishwa na nishati ya umeme kupitia mpango wa usambazaji umeme Vijijini.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la Ikungi Mashariki, Thomas Mgonto Kitima wakati akizungumza na Jambo Media kuhusu utekelezaji wa miundombinu mbalimbali, ikiwemo barabara, madaraja ,pamoja na umeme kutika Jimbo hilo.

Amesema Kata ya Siuyu Vitongoji vitakavyonufaika nufaika na huduma hiyo ya kuunganishiwa umeme ni pamoja na Kitongoji cha Isanga, Misimbo, Mundabi pamoja na Kitongoji cha Munindi ambvyo vyote vinakwenda kuwekewa umeme awamu hii.

Aidha Kwa Miundombinu ya barabara Mbunge Mgonto amesema ujenzi wa daraja la kimbwi ambalo awali lilikuwa na changamoto, ujenzi uaendelea kwa kasi na uko mbio kukamilika ili wananchi wanaotumia daraja hilo waweze kupita pasipo na shaka yoyote, huku madaraja mengine ya Magaire na Makote ambayo yote yanakwenda kukamilika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *