“Umeme ukikatika katikati ya safari abiria asiweze kugundua ”- Mkurugenzi TRC

Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Bwn. Masanja Kadogo amesema kuwa wameweka mfumo pacha wa Umeme katika treni hizo za Umeme kitu ambacho hata umeme ukikatika abiria hawatojua.

Kadogo amesema hayo leo mbele ya waandishi wa katika safari za majaribio ya treni ya umeme kati ya Dar es Salaam na Morogoro.”Tutaweka mfumo pacha wa umeme wa kawaida pamoja na dizeli ili umeme ukikatika katikati ya safari abiria asiweze kugundua chochote,” – Mkurugenzi TRC

Akaongeza “Watu wasiwe na wasiwasi kwamba umeme utazimia njiani, kuna ‘transmission’ ya kwetu peke yake kutoka gridi ya Taifa na ili treni iweze kusimama kwa ajili ya umeme basi mjue labda nchi nzima hakuna sehemu ya umeme.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *