Ulinzi umeimarishwa uliwemo wa Wanajeshi na Polisi katika Mahakama ya Kijeshi ya Makindye Nchini Uganda, ambapo mgombea nafasi ya urais mara nne, Dkt. Kizza Besigye anatarajiwa kufikishwa.
Hata hivyo, vyanzo vya Habari vimearifu kuwa Mahakama hiyo haitaketi leo kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Juu iliyoamuru kesi zote zinazowahusu raia katika Mahakama za Kijeshi zisitishwe mara moja.

Mahaka hiyo ilielekeza kuwa kesi hizo, zihamishiwe kwenye Mahakama za kiraia zenye mamlaka husika.