Ulevi watajwa kuwa chanzo cha Matukio ya mauwaji Jijini Dodoma

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya amesema matukio mengi ya mauaji na kujeruhiwa yanayoendelea katika Mkoa huo yanatokana na ulevi.

RPC Mallya ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya hali ya usalama katika mkoa wa Dodoma na kuongeza kuwa kwasasa wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi pamoja na kupeleka polisi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Sanjari na hayo RPC Mallya ameongelea suala la matukio ya ulawiti katika mkoa huo ambapo amesema kuwa kwasasa matukio hayo yamepungua kutokana na jitihada mbalimbali walizoziweka ikiwemo utoaji wa elimu kuanzia shuleni mpaka kwenye ngazi ya familia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *