Ukiajiri Raia wa Kigeni Faini,Unaweza Kufungwa Mika Mitatu

Na William Bundala,Kahama

Idara ya uhamiaji Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga imewataka wakulima wa tumbaku na pamba kufuata taratibu mpya zilizowekwa na idara ya uhamiaji nchini pindi wanapotoa ajira za muda(vibarua) kutoka nchi jirani.

Wito huo umetolewa leo na Afisa uhamiaji wa Manispaa ya Kahama Salum Rashid wakati akizungumza na Jambo Fm ofisi kwake kuhusu ajira za muda kwa vibarua kutoka nchi jirani kwenye mashamba ya Tumbaku na Pamba.

Rashid amesema kuwa manispaa hiyo ina wakulima wa Tumbaku na pamba ambao wanategemea vibarua kutoka nchi jirani hususan Burundi na kuwataka wafuate utaratibu kwa kuwaombea vibali kabla ya kuanza kwa msimu wa kilimo.

Ameongeza kuwa June 2023 Idara ya uhamiaji ilifanya maboresho kwenye sheria ya uhamiaji kwa kuanzisha kibali kipya mahususi kwa ajili ya vibarua wanaofanya kazi za msimu nchini Tanzania wanaotoka katika nchi jirani.

Sambamba na hayo Rashid amesema kuwa vibali hivyo vimeshaanza kutolewa nchini na mwenye jukumu la kuomba kibali hicho ni mwajiri na gharama zake zimegawanyika kwa muda wa miezi mitatu na miezi sita huku baadhi ya vibarua kutoka nchi ya Burundi wakiishukuru idara ya uhamiaji kuwa kuja na mpango kuwa hali waliyoelezea kwamba itawapa amani ya kufanya kazi kwa uhuru hapa nchini.

Kwa mujibu wa sheria ya uhamiaji sura ya 54 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2016 ukikamatwa umemuajiri raia wa kigeni bila kibali adhabu yake ni faini isiyopungua shilingi laki tano ama kifungo kisichozidi miaka mitatu au vyote kwa pamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *