UKAME: MSITUMIE NAFAKA KUTENGENEZA POMBE, TUNZENI CHAKULA – RC SENYAMULE

Na Gideon Gregory – Dodoma. 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule amewataka wananchi wa Mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanatunza chakula na wasitumie nafaka kwa ajili ya kutengenezea pombe kutokana na hali ya ukame inayoendelea nchini. 

RC Senyamule ametoa maagizo hayo hapa Jijini Dodoma, wakati akihitimisha kikao cha Kamati ya Ushauri ya mkoa (RCC), kilichokuwa kikijadili mambo mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo masula ya  elimu, kilimo pamoja na afya.

Amesema, “lakini pia nitumie nafasi hii kuwaagiza wananchi kuacha kutumia vibaya hakiba ya chakula walicho nacho ndani hivi sasa kwa kupika pombe na wale wenye mifugo wauze wakati huu ambao bado inaafya ili kiasi hicho cha fedha wanunue chakula na kujiwekea hakiba.”

Aidha, kutokana na hali hiyo inayoendelea kwasasa amewashauri wafugaji kuvuna mifugo na kununua chakula huku akieleza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa hata hiyo mifugo kukosa malisho kama hali ya hewa itaendelea hivyo.

Pia, amewaagiza viongozi wote wa Wilaya kwenda kutoa elimu kwa wananchi kuhusu utunzaji wa chakula wakati huu ambapo serikali ya mkoa endelea kuweka mikakati na kuona namna ya kukabiliana na hali hiyo.

Sambamba na hilo amehimiza juhudi za makusudi kuendelea kufanyika kwa kuwahimiza wakulima kulima kilimo cha umwagiliaji pale inapowezekana ili kufanikisha kupata mazao yanayostahili kulimwa sehemu hiyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi, Donald Mejeti, amesema kuwa licha ya uhaba wa mvua mwaka huu, pia yapo malalamiko ya wakulma kuuziwa mbegu ambazo hazikuota.

“Mheshimiwa Mwenyekiti yapo malalamiko kwa wanchi wetu kuwa wameuziwa mbegu ambazo hazijaota na mbaya zaidi inadaiwa kuwa mbegu zile zilkuwa na mkono wa serikali nimefutilia hadi kwa ofisa kilimo hakuna majibu.

Amesema hali hiyo inaingombanisha serikali na wananchi wakulima ambapo wananunua mbegu hizo kilo moja kwa Sh. 20,000 na wengine wametumia zaidi ya 200,000 lakini hakuna mbegu iliyoota na afisa kilimo wilayani wanamtisha kuwa afunge mdomo.

Naye, Katibu Tawala Msaidizi Sekta za Uzalishaji na Uchumi, Aziza Mumba amesema kiwango cha mvua kwa mkoa wa Dodoma mwaka huu ni hafifu na kwamba zimenyesha chini ya kiwango hali ambayo inatishia uhaba wa mavuno katika maneeo mengi, hivyo ipo haja kwa Wananchi kuanza kuchukua tahadhari.

“Kwa hali ilivyo sasa uhakika wa mavuno ni asilimia 48 ya amzao yaliyolimwa lakini kama ukame utaendelea wastani huu wa asilimia 48 utaendelea kushuka zaidi,” amesema. 

Akiongea katika kikao hicho Mbunge wa jimbo la Kongwa, Job Ndugai ametoa ushauri kwa Jiji kuona namna ya kufanya uwekezaji mkubwa ambao utabeba Mkoa mzima hasa kwa upande wa elimu.

Amesema, kutoka na Jiji kuwa na mapato nakubwa ina kila sababu ya kujenga shule kubwa ya bweni ambayo itaweza kuwahudumia wanafunzi wengi ambao watakuwa wamekosa nafasi katika shule za wilaya wanazoishi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *