Ukakamavu,Uzalendo Kupitia JKT Vimewafikia Vijana 52 119

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax amesema Wizara kupitia Jeshi Ia Kujenga Taifa (JKT) imeendelea kuwapatia vijana wa Kitanzania mafunzo ya ukakamavu, kuwajengea uzalendo na umoja wa kitaifa, na stadi za kazi ambapo idadi ya waliopatiwa mafunzo imeongezeka kutoka 26,000 Mwaka wa Fedha 2022/23 hadi kufikia 52,119 Mwaka wa Fedha 2023/24.

Waziri Dkt. Tax ameyasema hayo leo Mei 20,2024 Bungeni Jijini wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2024/25 na kuongeza kuwa kati yao wavulana ni 31,256 na wasichana ni 20,863.

“Aidha, vijana 12,000 wa kujitolea wanaendelea kupatiwa mafunzo katika makambi mbalimbali za JKT,amesema.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Stergomena Tax ameliomba Bunge Iiidhinishe kiasi cha Shillingi Trilioni 3. 32 katika Mwaka wa Fedha 2024/25.

Kipi ambacho huwezi kusahau ulichoahi kukutana nacho ukiwa katika mafunzo ya JKT?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *