UJENZI WA DARAJA LA BUGONGO BUSISI WAFIKIA ASILIMIA 99, KUWA KICHOCHEO CHA UCHUMI – MSIGWA


Katibu Mkuu wa Habari utamaduni sanaa na michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msingwa amesema kuwa ujenzi wa daraja la Bugongo busisi linalounganisha wilaya ya sengerema na Misungwi mkoani mwanza umefikia asilimia 99 tangu kuanza kwake na hivyo kwenda kuwa suluhu ya usafiri kwa wakazi wa ukanda wa ziwa na sehemu mbalimbali nchini.

Msigwa ameeleza hayo wakati akiwa Mkoani Mwanza akitembelea na kuangalia utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyopo katika mkoa huo akieleza kuwa mradi huo ni miongoni mwa miradi ambayo inakwenda kuchochea hali ya uchumi kupitia ukanda wa ziwa, kwani uchumi huo utashirikisha nchi jirani kama vile Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi na Uganda.

Aidha Msigwa amesema daraja hilo linakwenda kuwa suluhu ya wakati kwani awali wakazi wa mkoa huo walikuwa wakitumia zaidi ya saa 4 kwa kutumia kivuko na utakapokamilika daraja hilo litatumia dakika 3 kuvuka.

Mradi huo ambao unatarajiwa kutumia fedha kiasi cha zaidi ya Shilingi Bilioni 700 mpaka kukamilika kwake umebakiza asilimia 1 na kazi ndogondogo za kuukamilisha huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kuuzindua na kuanza kutumika rasmi.

“Hili ni daraja kubwa Afrika Mashariki na Kati na ni daraja kubwa namba 6 Barani Afrika ambalo nchi nyingi za Afrika zitakuja kujifunza hapa, mana hapa ni kama tumeunganisha kisiwa na kisiwa hili ni jambo kubwa sana,” amesema Msigwa.

Pamoja na hayo Msigwa amesema daraja hilo hilo litakuwa ni daraja la muda mrefu litakalotumika kwa muda miaka 100 huku uwezo wake wa kubebe mizigo ukiwa ni tani 160.

“Serikali ya awamu ya sita wakati inaingia madarakani mradi huu ulikuwa na asilimia 25 na sasa imekamilisha mradi huu kwa asimilia 99 hivyo kimsingi mradi huu umekamilika”. amesema Msigwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *