
Uingereza imewawekea vikwazo wanasiasa kadhaa wa Uganda akiwemo spika wa bunge la nchi hiyo Anita Among kufuatia madai ya ufisadi
Serikali ya Uingereza imesema hii ni mara ya kwanza kutumika kwa sheria yake mpya ya kimataifa ya vikwazo dhidi ya ufisadi kwa watu wanaokabiliwa na madai ya ufisadi nchini Uganda, na kwamba ni sehemu ya msako wa kimataifa.
Among, ni mmoja wa watu watatu wanaolengwa na vikwazo vya usafiri vya Uingereza pamoja na kufungiwa kwa mali zake,Walengwa wengine wawili ni Mary Goretti Kitutu na Agnes Nandutu waliokuwa mawaziri wanaohusika na eneo masikini la mpaka wa Uganda la Karamoja.

Taarifa iliyotolewa na bunge la Uganda imesema vikwazo hivyo vinatokana na kile ilichotaja kuwa dhana potofu na Taarifa hiyo pia imesema kuwa Among hajawahi kushitakiwa kwa ufisadi katika mahakama yoyote ya kisheria kinyume na dhana inayoibuliwa katika taarifa iliyotolewa na Uingereza.
Kitutu na Nandutu walikabiliwa na madai ya kuiba mabati ya nyumba yaliokusudiwa kutumiwa na watu maskini chini ya mradi unaofadhiliwa na serikali ya Uganda.