Uingereza kuanza kuwapeleka wahamiaji Rwanda Julai Mosi

 Serikali ya Uingereza imeiambia Mahakama Kuu mjini London kwamba safari za kwanza za ndege za kuwahamishia waomba hifadhi nchini Rwanda zitaanza kati ya Julai Mosi na Julai 15.

Jaji Martin Chamberlain alifichua tarehe hizo alipokuwa akipanga kusikilizwa kwa pingamizi lijalo la kisheria kwa sheria hiyo mpya ya uhamiaji.

Pingamizi hilo liliwasilishwa na chama cha wafanyakazi wa umma nchini humo na Sheria mpya ya uhamiaji nchini Uingereza inaruhusu mawaziri kupuuza sehemu za sheria za ndani na za kimataifa wakati wa kuamua juu ya uhamishaji huo wa lazima kwa waomba hifadhi.

Awali Aprili 22, Waziri Mkuu Rishi Sunak alisema kwamba alitarajia safari za kwanza za ndege kuondoka  ndani ya wiki 10 hadi 12 lakini hakutoa tarehe kamili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *