Na Frank Aman – Geita.
Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Geita (TPF-NET) na Jeshi la Polisi limepongezwa kwa jitihada kubwa za kukabiliana na kuzuia uhalifu kwenye jamii na kufanya Geita kuendelea kuwa salama.
Hayo yamebainishwa katika Manispaa ya Geita na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba alipozungumza na Wakaguzi na Askari wa Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoani Geita wakati wakiendelea na majukumu mbalimbali kwenye jamii kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka 2025.

“Ninaona mlivyo imara kwenye kuimarisha usalama, kwa hakika ninyi ni watu hodari kweli kweli. Taifa letu lipo salama chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Chini ya Kamanda Jongo usalama wa raia na mali zao uko salama kwa sababu ninyi Askari wa kike mpo mstari wa mbele, hongereni sana,” amesema Komba.

