UGENI CHUMBA CHA MAITI KUJIFUNZA THAMANI YA MAISHA

Unapojikuta kwenye treni isiyo sahihi, usisite kushuka kwenye kituo cha kwanza kabisa kwani kadri unavyoendelea kukaa, ndivyo utakavyosogea mbali zaidi kutoka mahali unapokusudia kuwa na safari ya kurudi itakua ngumu na ya gharama kubwa zaidi.

Lakini hii sio tu kuhusu treni, bali inahusu pia maisha, kwa kuwa unapoelekea kwenye njia mbaya iwe katika uhusiano, kazi, au chaguo ambalo umefanya itambue mapema na uwe na ujasiri wa kuondoka, kiufupi fanya mamuzi ya mapema kwa kila jambo na tanguliza umakini.

Unapogeuka haraka, ndivyo itakavyokuwa rahisi kutafuta njia ya kurudi mahali unapotaka kuwa kweli sababu katika maisha kuna mambo mengi tunayakosea ambayo laiti tungetambua mapema au kuchukua maamuzi mapema basi tungefanikiwa kuepuka matatizo zaidi lakini tukipata na funzo.

Hata hivyo, binadamu huwa tuna matatizo maana mara nyingi hatukubali ushauri au kujishughulisha kutafuta ukweli wa mambo, na wakati mwingine tumekuwa tukidharau vitu au kuwadharau watu na kujiona tumemaliza kila kitu maishani.

Hivyo, hapa nakupa ushuhuda na mbinu zitakazokufanya utambue siri ya maisha kiasi ukajiheshimu na kuwaheshimu wengine.

1. Kuna Mtu alishawahi, hivyo nawe tembelea Chumba cha Maiti, ili utambue thamani ya maisha.

2. Kutembelea Hospitali kutakufanya uthamini afya yako na thamani ya utu.

3. Kutembelea Gereza kutakufanya uthamini uhuru ulionao.

4. Mambo unayofurahia na kuyachukulia ni ya kawaida, wengine hawana na wanayahitaji hivyo jikubali jinsi ulivyo.

5. Kila siku kila saa mshukuru MUNGU kwa mambo mazuri aliyokutendea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *