Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Uganda wasitishiwa misaada kisa Ushoga

Benki ya Dunia imetangaza kusitisha utoaji wa mikopo mipya kwa Serikali ya Uganda baada ya kujiridhisha kuwa sheria ya Nchi hiyo inayopinga ushoga ambayo imelaaniwa na Mataifa mengi ya magharibi ikiwemo Marekani pamoja na Umoja wa Mataifa, inakinzana na maadili ya Beki hiyo.

Timu ya Benki ya Dunia ilisafiri hadi nchini Uganda mara baada ya sheria hiyo kupitishwa mwezi Mei 2023 na kuamua kuwa hatua za ziada zilihitajika ili kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya kimazingira na kijamii vya Benki ya Dunia, sheria hiyo mpya ya Uganda inatoa hadi hukumu ya kifo kwa ‘ushoga uliokithiri’ ikiwemo kusambaza Virusi Vya Ukimwi kupitia ngono ya mashoga.

Rais mpya wa Benki ya Dunia, Ajay Banga ambaye alichukua wadhifa huo Mwezi June, amesema hakuna ufadhili mpya wa umma utakaotolewa na Benki hiyo kwa Uganda hadi hatua za ziada na za ufanisi zitakapochukuliwa, na kuongeza kuwa hatua hizo sasa zinajadiliwa na Serikali ya Uganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *