Ucheleweshwaji wa fedha za utekelezaji wa mkataba wa lishe,baadhi ya idara kutopanga utekelezaji wa mkataba huo,baadhi ya vijiji na mitaa kutofanya maadhimisho ya siku ya lishe na kutokuwapo kwa utaratibu wa kufanya usafi kila mwisho wa mwezi katika baadhi ya halmashauri ni miongoni wa changamoto zilizoathiri utekelezaji wa mkataba wa lishe Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh.Christina Mndeme ameyabainisha hayo leo Agosti 9,2023 wakati akifungua kikao tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe kwa mwaka wa fedha 2022|2023 na kubainisha kwamba kwa mujibu wa
“ Takwimu za lishe zilizotolewa na Wizara ya Afya kupitia Utafiti wa Taifa wa Masuala ya Afya na Lishe wa mwaka 2022 umeonesha kuwa udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano umepungua kutoka asilimia 32.1 hadi asilimia 27.5,ukondefu kutoka asilimia 4.3 hadi asilimia1.3, hii inaonesha kuwa juhudi zetu za kupambana na utapiamlo zinazaa matunda”amsema Mh. Mndeme
Ili kuondokana na changamoto zilizoathiri utekelezaji wa mkataba wa lishe kwa mwaka wa fedha 2022|2020 ameagiza changamoto zote kutatuliwa na fedha kutolewa kwa wakati na halmashauri zote kuhakikisha ajenda ya lishe inakuwa ya kudumu katika vikao vyote vya halmashauri.
Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kimehudhuriwa na wakuu wa wilaya,wakurugenzi wa halmashauri,makatibu tawala wasaidizi,wajumbe wa kamati za usimamizi wa Afya mkoa waganga wa halmashauri,wakuu wa Idara,maafisa lishe wa halmashauri na wadau wa maendeleo.