UCHAGUZI KUTOFANYIKA NI KUVUNJA KATIBA – MAKALA

Na Saada Almasi  – Simiyu. 

Wananchi mkoani Simiyu wametakiwa kutoa hofu juu ya tetesi za kutofanyika kwa uchaguzi mkuu ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu kwani suala hilo litakuwa ni kuvunja katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Hayo yamebainishwa na Katibu Uenezi na Itikadi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ACP Amos Makala  alipokuwa akihutubia wananchi hao waliompokea wilayani Bariadi katika uwanja wa soko la zamani mara baada ya kupita wilaya ya Busega akitokea mkoani Mwanza

” tumekuja kuwakumbusha na kuwaandaa kuhusu uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu upo kwani unafanyika kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inaeleza kila baada ya miaka mitano kufanyike uchaguzi wa kuchagua viongozi tunaowataka” amesema Makala.

“Na safari hii hakutokuwa na wagombea kupita bila kupingwa viongozi wote watapigiwa kura ya halali na washinde kihalali ,na ninaamini wote mko tayari kwa uchaguzi ” ameongeza Makala 

Sambamba na hilo Makala amesema kuwa vyamba 17 vya upinzani pekee ndivyo vitakavyoshiriki katika uchaguzi kutokana na chama kikuu wa upinzani CHADEMA kutoshiriki uchaguzi japokuwa madai yaliyowekwa mezani na chama hicho ya kutokuwa na Tume huru ya uchaguzi si ya kweli.

Amesema, hadi sasa sheria za tume hiyo zinaelwza namna ya upatikanaji wa wajumbe wake badala ya kuteuliwa na raisi sambamba na kutopewa wakurugenzi  jukumu la kusimamia uchaguzi huo.

” mwaka huu vinatarajia vyama 18 kushiriki katika uchaguzi ambapo 17 vikiwa ni upinzani ,wenzetu CHADEMA hawatoshiriki maana wamesusia mechi kwa kuogopa kuingia uwanjani sasa madai yao ya kutokuwa na Tume huru si ya kweli.

Tume huru ya Taifa itakuwepo na wajumbe wake watachaguliwa kupitia mchakato wa kuomba nafasi hizo na baadae jaji mkuu atawaidhinisha tofauti na awali ambapo raisi alieateua ,lakini pia uchaguzi awali ulisimamiwa na wakurugenzi lakini sasa utasimamiwa na viongozi wa umma kwa hiyo msiwe na wasiwasi ” ACP Makala

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *