UBORA WA MIRADI TABORA WAMPA TABASAMU KIONGOZI MBIO ZA MWENGE

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu wa 2025, Ndugu Ismail Ali Ussi ameeleza kukoshwa na ubora wa miradi ya maendeleo iiliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora. 

Ussi ametoa maelezo hayo, wakati alipotembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Manispaa ya Tabora.

Ikumbukwe kuwa, Wilaya ya Tabora imeupokea Mwenge wa Uhuru na kuukimbiza jana Julai 30, 2025 ambapo Mwenge wa Uhuru umeangazia miradi minane yenye thamani ya zaidi ya bilioni kumi na tisa (19) katika kata za Itetemia, Kitete, Ipuli, Mtendeni, Isevya, Misha pamoja na Cheyo. 

Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa na Mwenge wa Uhuru ni Kituo cha Afya Itetemia, Kikundi cha Vijana cha asilimia kumi cha KAZI DIGITAL, Barabara ya Maili Tano, Kiwanda cha Kuchakata Nishati Mbadala cha Gereza Kuu la Uyui, Ofisi ya Kata ya Isevya, Chanzo cha Maji cha Bwawa la Igombe, pamoja na madarasa ya Wanafunzi wenye mahitaji maalumu shule ya Sekondari Kazima.

Ndugu Ismail Ali Ussi kwa nyakati tofauti tofauti akiongea na Wananchi kwenye miradi na maeneo ya ujumbe wa Mwenge wa uhuru, amewaomba na kuwahimiza kuendelea kuwa wazalendo, kuchapa kazi, kuchukua tahadhari dhidi ya maradhi kama Malaria na UKIMWI, na kubwa zaidi akisisitiza wananchi kujitokeza kuwachagua viongozi wanaowapenda ifikapo Oktoba mwaka huu kwa utulivu na amani. 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe. Upendo Wela amemshukuru Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Ismail Ali Ussi kwa kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo iliyopo katika Manispaa ya Tabora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *