Uapisho wa Rais mteule wa Marekani, Donald Trump anatarajia kufanyika hii leo Januari 20, 2025 ndani ya jengo la Bunge la Capitol.
Trump ambaye atakuwa rais wa 47 wa taifa hilo kubwa duniani anarudi White House kwa mara ya pili baada ya kuongoza kwa muhula mmoja akiwa rais wa 45 kati ya mwaka 2017 hadi 2021.

Kutokana na baridi kali, hii itakuwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 40 kwa rais mteule kuapishwa ndani ya jengo badala ya eneo la wazi tangu mwaka 1985 wakati Rais Ronald Reagan alipoapishwa ndani ya jengo .


