Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan katika Picha ya pamoja na Mtanzania Steven Magombeka Maarufu Kama Kasampaida ambae hivi karibuni alishinda Tuzo ya Vijana Wenye Ushawishi Barani Afrika, akikabidhi Tuzo hiyo kwa Rais Ikulu ya Chamwino Dodoma leo April 29, 2025.

Itakumbukwa Kijana Magombeka alishinda Tuzo hiyo tarehe 12 ya mwezi April 2025 jijini Accra Nchini Ghana na Leo hii ameiwasilisha tuzo hiyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kama shukrani kubwa kwa mchango wake wa kuendelea kuwainua Vijana mbalimbali katika sekta mbalimbali Nchini.
Aidha Ndg, Magombeka amemkabidhi Rais Samia Zawadi ya Picha aliyompiga mnamo February 15,2024 wakati wa ziara Nchini Norway kama sehemu ya Kumbukumbu ya Picha alizowahi kumpiga Rais.

Tuzo hizi mashuhuri zinawatambua Vijana wajasiriamali bora, wanaharakati, waleta mabadiliko na wafuatiliaji ambao wameonyesha ubora wa kipekee katika nyanja zao Kukiwa na takriban uteuzi wa vijana 5,000 kutoka nchi 52 za Afrika.
Pongezi za dhati kwa Vijana 100 Wenye Ushawishi Zaidi wa 2025! Mafanikio yako bora yanaendelea kutia moyo na kuleta mabadiliko katika bara zima na kwingineko.
