Na Gideon Gregory, Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema wanaendelea kufanya tathmini pale ambapo watagundua bado kuna kundi ambalo halipati fursa ya kupata mkopo linaweza kupata huku wakiendelea kuweka utaratibu kupitia mifuko waliyonayo hata ndani ya Serikali waweze kupata fursa hiyo.
Waziri Mkuu ameyabainisha hayo leo Februari 13,2025 Bungeni hapa Jijini Dodoma wakatia akijibu swali la Mbunge wa Hai Saashisha Mafuwe aliyehoji Serikali haioni sasa ni wakati sahihi wa kufanya marekebisho ya kikanuni ili kundi wanaume nao wanufaike na mikopo bila kigezo cha umri.
“Kwahiyo tutaendelea kuboresha utoaji mikopo kwa makundi yote ili yaweze kupata fursa ya kupata mitaji na kuendesha shughuli za kiuchumi,”amesema.
Amesema upatikanaji wa fursa za mikopo katika maeneo mbalimbali, ulifanyiwa tathmini na wakagundua kwamba yako makundi ambayo hayana fursa nzuri yana fursa ndogo ya kupata mikopo hiyo.
“Haya ni makundi ambayo baadae tuliyaanzishia mikopo maalum kupitia Halmashauri zetu nao ni walemavu, wananwake na vijana”,amesema.
Ameongeza kuwa kundi hilo waliamua kuanzisha mfuko maalum kwenye Halmashauri ili lipate nafasi ya wazi ya kupata mikopo kwenye maeneo yao, hivyo swala la wanaume kupata nafasi hao ndiyo walikuwa wapate nafasi ya wazi kunufaika na hata baada ya kubadilisha umri bado na wao wana nafasi kubwa wakati huo.
“Vijana wakati wanafikia umri wa miaka 35 wanaume ambao ni vijana wanapata nafasi ya kukopa wakiwa vijana lakini baada ya miaka 35 walikuwa na fursa ya kwenda kuingia kwenye taasisi za kifedha na ndiyo fursa ambayo tulifanya tathmini tukagundua kwamba wengi wanaopata mikopo kwenye taasisi mbalimbali za kifedha ni wanaume kuliko wakina mama,”mesema.
Aidha, amesema hata baada ya kubadilisha kigezo cha kijana kutoka miaka 35 mpaka 45 bado anakuwa mtu mzima anawaeza kupata mkopo vilevile na kundi hili bado lina nafasi ya kupata mkopo kutoka katika taasisi mbalimbali lakini pia kwenye Halmashauri.