Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Tuoneshe Mshikamano Kwa Wakimbizi

Dunia leo inaadhimisha siku ya wakimbizi, kauli mbiu ikiwa ni mshikamano na wakimbizi,Serekali,Mashirika mbalimbali ya kiserekali na binafsi Duniani kote huungana na shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR katika dhima ya kuangazia hali za watu wanaokimbia mataifa yao kwa sababu ya matatizo mbalimbali.

Migogoro inayosababisha vita imekuwa chanzo kikubwa cha kuzalisha wakimbizi na kujikuta katika kambi ndani na nje ya mataifa yao, baadhi yao wanaendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali za hali zao za ukimbizi.

Kwa mujibu wa Ripoti ya hali ya mwenendo wa wakimbizi duniani ya mwaka 2024  (2024 Flagship Global Trends Report) ya UNHCR inaeleza kwamba kiwango cha ongezeko la wakimbizi kimefikia kiwango cha kihistoria na kwa mwaka jana na mwaka huu,migogoro inayoendelea katika maeneo mbalimbali duniani kote imefanya hali kuwa mbaya.

Hadi mwezi Mei 2024, dunia imeshuhudia ongezeko la watu milioni 120 waliolazimishwa kukimbia makazi yao, ikiwa ni ongezeko la 12 mfululizo kwa kila sababu kubwa ya ongezeko maradufu la wakimbizi, UNHCR inasema ni mgogoro wa Sudan ambao umechangia raia milioni 10.8 kuwa wakimbizi mpaka mwishoni mwa 2023.

Katika mataifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na Myanmar, mamilioni ya watu walikimbia makazi yao kwa mapigano ambapo inakadiriwa mpaka mwishoni mwa mwaka jana hadi watu milioni 1.7, sawa na asilimia 75 ya idadi ya watu wa mataifa hayo waligeuka kuwa wakimbizi aidha vita mbaya ya ukanda wa Gaza vimeongeza wakimbizi wa Palestina, na Syria na kufikia milioni 13.8.

Aidha ripoti ya UNHCR inaonyesha duniani kote zaidi ya wakimbizi milioni moja walirejea kwao katika kipindi cha mwaka jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *