TUNZENI MIUNDOMBINU YA BARABRA – RC MACHA

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, amezitaka mamlaka husika na jamii kwa ujumla kutunza  miundombinu ya barabara, ili  iweze kudumu kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja barabra hizo kuendelea  kuwahudumia   wananchi na kurahisisha sekta ya usafirishaji.

RC Macha Ameyasema hayo leo Februari 26, 2025 wakati akifungua kikao cha Bodi ya Barabara kwa  mwaka 2025 kilichoketi leo katika ukumbi wa mikutano  wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga

Amesema, Serikali imefanya kazi kubwa ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, lakini katika mkoa wa Shinyanga kuna tatizo la kutozitunza barabara hizo.

“Katika Mkoa wa Shinyanga tusipomshukuru Rais Samia juu ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja,tutakuwa wachoyo wa fadhira,lakini tunakabiliwa na changamoto ya utunzaji wa barabara,” amesema Macha.

Ameongeza kuwa, “Barabara zetu ukiangalia mitaro imejaa takataka, imeota majani, chupa za maji zimetupwa umo,na mvua zikinyesha maji yanakosa pakupita na kusababisha kingo kuanza kubomoka.”

Aidha, ametolea mfano wa barabara ya Nyamilangano iliyopo katika halimashuri ya   Ushetu wilayani Kahama,kwamba barabara hiyo ni mpya lakini mitaro yake imaanza kujaa uchafu.

RC Macha pia ameonya tabia ya baadhi ya watu  waache wanaochimba  mchanga kando ya hifadhi ya barabara, na kuigusia barabara ya Nyamilangano iliyopo Ushetu, kwamba tayari mashimo yameanza kukata  barabara.

“TARURA,TANROADS na Wakurugenzi wa Halmashauri acheni kuandikiana barua kwenye suala la utunzaji wa barabara,itaneni mkae kwenye vikao na kujadili kwa pamoja juu ya utunzaji wa barabara hizi, sababu kila mmoja ukimuuliza mnasukumiana nilishamwandikia barua flani, hiyo sitaki kaeni vikao,” amesema.

Ametahadharisha pia watu ambao wanapewa Vitalu vya kuotesha miche kando ya hifadhi ya barabara, au kufanya shughuli zingine, kwamba wapewe mikataba pamoja na uangalizi mkubwa, ili wasije kujenga makazi ya kudumu na hata kupelekewa huduma za kijaamii, yakiwamo maji na umeme, na mwisho wasiku wanakataa kuondoka kuwa maeneo hayo ni ya kwao.

Amegiza pia uwepo na usimamizi mzuri kwa Wakandarasi ambao wanajenga barabara hasa wakati wa kumaliza kazi zao,kuwa wazimalize kwa ufanisi na siyo kulipua, sababu kuna baadhi ya barabara amekuwa zikimalizika zikiwa na mwisho mbovu.

Pia, amegusia suala la Wakandarsi kuweka vifusi kwenye barabara na kisha kutokomea kwa muda mrefu, kwamba tatizo hilo nalo liangaliwe ili kutozuia shughuli za kiuchumi kutofanyika kwa wananchi sababu ya vifusi hivyo.

Amesisitiza pia suala la mikataba na Wakandarasi liangaliwe pale wanapokwenda kuchimba mashimo kwenye maeneo ya watu, kuwa wakimaliza shughuli zao waone namna ya kuyafukia, au kuweka mazingira mazuri mashimo hayo yatumike kwenyeshea maji mifugo,kufugia samaki,na siyo kuachwa hovyo na hata kusababisha maafa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *