LISSU ASHINDA UENYEKITI CHADEMA, MBOWE AKUBALI MATOKEO

Kupitia ukurasa wake wa X, Freeman Mbowe amechapisha andiko linaloonesha kuwa amekubali ushindi wa Tundu Lissu kuwa Mwenyekiti mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Mbowe ameandika kuwa, “Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya Uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama chetu CHADEMA uliohitimishwa leo asubuhi 22 Januari 2025. Nampongeza Mhe. Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la Uongozi wa Chama.” Freeman Mbowe.

Hata hivyo, matokeo rasmi ya nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA ni kama ifuatavyo:

1014 zilizojisajili
999 kura zilizopigwa
Kura halali 996
Kura zilizoharibika 3

MATOKEO:

Odero Charles kura 1 = 0.1%
Freeman Mbowe kura 482 = 48.3%
Tundu Lissu kura 513 = 51.5%

Aidha, mshindi wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti CHADEMA Bara ametangazwa kuwa ni John Heche ambaye amepata kura 577 akiwashinda wapinzani wake Ezekia Wenje aliyepata kura 372 na Mathayo Gekul aliyepata kura 49.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *