Mkutano wa Mifumo ya Chakula Barani Afrika, umefunguliwa rasmi na Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango. Mkutano huo unaofanyika mkoani Dar es Salaam utafikia tamati Septemba 08, 2023.
Pamoja na mambo mengine mkutano huo unajadili masuala mbalimbali kuhusu uhakika wa chakula Barani Afrika na umejumuisha washiriki zaidi ya elfu tano huku wawasilisha mada wakiwa zaidi ya 350.