TUNAFUATILIA SAKATA LA MWENEZI MLIGO, TUTACHUKUA HATUA – CHADEMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kinafuatilia kwa karibu na kinafanya uchunguzi wa kina juu ya tuhuma zinazosambazwa mitandaoni kuhusu madai ya kupigwa kwa Mratibu wa Uenezi wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA), Sigrada Mligo, ili kubaini ukweli wa jambo hilo na kuchukua hatua stahiki.

Taarifa iliyotolewa hii leo Machi 31, 2025 na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia imeeleza kuwa wanafuatilia kwa makini njama za Chama cha Mapinduzi (CCM), za kutumia tukio hili kwa manufaa yao.

“Tunatoa wito kwa Mh. Sigrada Mligo kuwa makini na mahusiano yake na CCM ili kuepuka kutumiwa kwa malengo yasiyo na nia njema, ambayo yanaweza kuathiri si tu hadhi ya Chama bali na ya kwake pia kama kiongozi na usalama wake binafsi,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, Viongozi wa BAWACHA Kanda ya Kati na Mkoa wa Dodoma wamefika Hospitali ya Benjamini Mkapa kumjulia hali Mwenezi Sigrada Mligo aliyelazwa baada ya kuhamishwa kutoka Hospitali ya Mkoa wa Njombe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *