TUNACHUNGUZA UKWELI WA TAARIFA TA KUTEKWA KWA POLEPOLE – POLISI

Jeshi la Polisi Nchini, limeuarifu umma kuwa kuwa linachunguza ukweli wa taarifa zinazosambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii na ndugu wa aliyekuwa Balozi w Tanzania Nchini Cuba, Humphrey Polepole anayedaiwa kutekwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hii leo Oktoba 6, 2025 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Makao Makuu Dodoma imeeleza kuwa wameanza kufanyia kazi taarifa hiyo, ili kubaini ukweli.

Hata hivyo, taarifa hiyo imeongeza kuwa bado Jeshi la Polisi linaendelea kumsubiri Polepole aripoti katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai.

Hivi karibuni Humphrey Polepole alitumiwa barua ya wito wa kuripoti Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, ili atoe maelezo kuhusiana na tuhuma mbalimbali alizozitoa kupitia Mitandao ya Kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *