Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, amesema kwamba chama chake kinamini kuunda serekali kwa
kutumia Falsafa Jumuishi ambayo haitabagua vijana wakizanzibari kutokana na itikadi na imani za vyama vyao vya siasa.
Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ameyasema hayo viwanja vya Stela Daraja bovu Jimbo la Welezo wilaya ya Maarib A Unguja alipohutubia wananchi na wanachama wa chama hicho katika mkutano wa hadhara.
![](https://jambofm.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/othman.jpg)
Amesema, Vijana hawapaswi kufanya makosa ya kutokiuna mkono chama hicho kwamba chama chake kinakusudia kuinyoosha nchi na kuwakabidhi vijana ili washindane katika kuipeleka mbele nchi yao kwa kuwa ubaguzi hauwezi kusaidia katika kujenga maendeleo ya taifa.
Othman ameongeza kuwa, ni muhimu kujenga utawala mwema utakao heshimu maamuzi ya wananchi kwa kuwa ufalme wa nchi ni Wananchi wenyewe na kwamba ndio wenye maamuzi juu ya namna wanavyotaka nchi yao iendeshwe.