TUMIENI MFUMO WA MANUNUZI WA NEST – RAS NGOMA.

Wadau wa manunuzi Nchini wamehimizwa kutumia mfumo wa manunuzi wa Kiserikali wa kielektroniki (NEST) ili kuimarisha uwazi katika mchakato wa kupata wazabuni wenye gharama nafuu zinazoendana na bajeti ya serikali.

Hayo yameelezwa na katibu tawala msaidizi mkoa wa Mwanza, Chagu Ngoma wakati akimwakilisha mkuu wa mkoa wa mwanza katika warsha ya kuwajengea uwezo zaidi ya wadau 200 wa ununuzi nchini kutoka kwenye taasisi na mashirika mbalimbali ya umma ambapo amesema katika mchakato mzima wa kupata wazabuni ni lazima wadau wa ununuzi hapa nchini watumie mfumo wa kielekroniki yaani nest ili kurahisisha mchakato wa ununuzi.

“Mfumo huu umeletwa mahsusi ili kusaidia kuongeza wigo wa ushiriki wa wazabuni, kukidhi mahitaji na matarajio ya watumiaji pamoja na kurahisisha mchakato wabuombaji zabuni hivyo nendeni mkazingatie hayo ili kulisaidia taifa.” Mhandisi chagu.

Katika hatua nyingine chagu pia ametoa wito kwa mamlaka ya ununuzi wa umma ppra kuendelea kuboresha mfumo huo ikiwa ni pamoja na  kuweka mazingira rafiki kwa wazabuni na kutoa mafunzo kwa taasisi za ununuzi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

kwa upande wake meneja wa kujenga uwezo na huduma za ushauri kutoka mamlaka ya PPRA Nchini, Bw. Gilbert Kamule amesema kwa sasa mfumo wa NEST unasaidia kupunguza muda wa mchakato wa manunuzi huku pia ukisaidia kupunguza gharama.

Nao baadhi ya wadau wa ununuzi hapa nchini walioshiriki katika mafunzo hayo wamesema kabla ya mfumo wa NEST haujaanza kutumika walikua wanapitia changamoto mbalimbali ikiwemo mchakato wa manunuzi kuchukua muda mrefu hasa katika maswala ya kimkataba ila kwa sasa ujio wa mfumo huu utakwenda kurahisisha uendeshaji wa shughuli zote za manunuzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *