‘Tumejadili wananchi wa Afrika Mashariki kunufaika na fursa zao’ – Rais Samia

Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuzungumza na wagenu wake ambao ni Rais wa Kenya William Ruto na Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametoa taarifa juu ya mazungumzo yao na sababu ya wao kukutana.

Rais samia amesema ‘Nimekuwa na wakati mzuri jana Ikulu ndogo, Tunguu Zanzibar, nikiwa na Mheshimiwa Rais Yoweri Museveni na Mheshimiwa Rais William Ruto’ – Rais Samia

‘Pamoja na mambo mengine tumejadiliana kuhusu;-

‘1. Kuongeza kasi ya kupatikana kwa Shirikisho la Afrika Mashariki’ – Rais Samia.

‘2. Hatua za kuchukua na kutekeleza ili kuhakikisha wananchi wa eneo la Afrika Mashariki wananufaika na faida za kiuchumi kwa soko na fursa tulizonazo’ – Rais Samia

‘3. Umuhimu wa ulinzi na usalama kama moja ya nguzo muhimu kutuwezesha kufikia yale tunayokusudia.’ – Rais Samia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *