TUMEIFUNGUA NCHI KIBIASHARA, UWEKEZAJI – RAIS SAMIA

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kutafuta masoko ya ndani na nje ya nchi kwa ajili ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi, akisisitiza kuwa Tanzania imefungua milango zaidi kwa biashara na uwekezaji.

Rais Samia amesema hayo leo, Agosti 8, 2026, wakati akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya John Malecela, Nzuguni, Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo Maalum kutoka kwa Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, kwa niaba ya Kamati ya Maandalizi ya Nanenane Kitaifa, 2026 katika viwanja vya Maonesho vya Dkt. John Samuel Malecela, Jijini Dodoma, Agosti 8, 2026.

Amesema hatua hiyo inalenga kuwawezesha wazalishaji kupata masoko ya uhakika huku ikiendelea kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

“Tumeifungua nchi kibiashara na uwekezaji na tunaendelea kuvutia wawekezaji wa ndani na nje, sambamba na mwelekeo wa Dira yetu ya Taifa unaoipa sekta binafsi asilimia 70 ya utekelezaji wake,” amesema Rais Samia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *