Mjumbe wa Tume ya Uchunguzi wa ghasia wakati na baada ya uchaguzi, Prof. Ibrahim Juma amesema, ripoti haijataja majina ya wahusika kwasababu za kisheria.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 28, 2026, amesma wahusika wangeweza kwenda mahakama kuu na kuchukua hatua za kuiamuru tume kufuta aya zote zilizowataja kwenye ripoti kwasababu hawakupewa haki ya kusikilizwa.
“Mhusika ambaye angetajwa angeomba amri na aya zote tunazomtaja bila kumpa nafasi ya kuusikilizwa zingefutwa kwenye ripoti.

“Katika Mahakama ya Kenya imeshawahi kufanya hivyo na Mahakamu ya Juu ya Canada imeshawahi kukutana na hoja hiyo kwamba kuna watu walitajwa na tume lakini hawakupewa nafasi ya kusikilizwa ikabidi aya zote zinazowatajwa ziondolewe,” amesema Prof. Ibrahim.
Amesema hivyo tume ilichukua tahadhari hiyo kutokana na walichukua uzoefu walionao.


