TUHUMA ZA WIZI: MWANAFUNZI MBARONI KWA MAUAJI KILIMANJARO

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia mwanafunzi mmoja wa Kidato cha Tatu (17), kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kitu chenye ncha kali mwanafunzi mwenzake na kusababisha kifo chake katika Shule ya Sekondari Kisarika.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, SACP Simon Maigwa, tukio hilo limetokea Agosti 28, 2026, baada ya kutokea ugomvi baina ya wanafunzi hao kufuatia tuhuma za kuibwa kwa vitu mbalimbali katika mabweni ya shule.

Mwanafunzi aliyejeruhiwa alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mawenzi.

Polisi wamesema uchunguzi wa kina unaendelea ili kukamilisha taratibu za kisheria na kumfikisha mtuhumiwa mahakamani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *