Na William Bundala, Kahama – Shinyanga.
Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB) Mkoa wa kitumbaku Kahama imewataka wakulima wa zao la Tumbaku katika mkoa wa kitumbaku Kahama,Kuhakikisha wanang’oa mabaki ya magugu ya tumbaku, ili kuzuia magojwa na wadudu wanaoshambulia zao hilo.
Kauli hiyo imetolewa na kiongozi wa bodi ya tumbaku Kahama Lucas Mihayo wakati akizungumza na wakulima wa tumbaku katika kata za Bulungwa na Ubangwe kwenye semina ya kuwajengea uwezo namna ya ufungaji bora wa tumbaku kwa kuzingatia madaraja.
Mihayo amesema kuwa baada ya kuvuna tumbaku wakulima wanatakiwa kung’oa masalia ya zao hilo ili kuepusha magonjwa na wadudu ambao wanaweza kuhama kutoka shamba moja hadi lingine.

“Wakulima wengi mkimaliza kuvuna mnaacha kung’oa magugu ya tumbaku na wengine mnakata na kuacha visiki,hii njia si sahihi kikubwa mnatakiwa kung’oa kabisa kuchoma moto masalia yote baada ya kuvuna” Amesema Mihayo.
Sambamba na hayo Mihayo ametoa wito kwa wakulima Kutenga maeneo mengi ya kusia mbegu ili pale walipopanda mbegu msimu huu,wasipande tena ili kungo kwa kuipumzisha ardhi na kuwaauwa wadudu wanaoharibu zao la Tumbaku.
“Jambo lingine niaombe sana wakulima,tuwe na maeneo mengi ya kusia mbegu zetu,ili kila mwaka unahama hapo ulipolima unaenda kulima sehemu nyingne,hii itasaidia kulipa shamba rutuba na kuuwa wadudu” Ameongeza Mihayo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushrika Kahama (KACU) amesisiza kuhusu usimamizi wa kufunga tumbaku huku akitoa wito kwa viongozi wa vyama vya msingi kushiriki kikamilifu katika zoezi la ufungaji wa Tumbaku ili kuhakikisha wakulima wanafunga tumbaku bora kwa kuzingatia masharti ya bodi na wanunuzi.
“Msimu wa masoko umefika,niwaombe sana vingozi wenzangu tutembee kwa wakulima ili kusimamia ufungaji bora wa tumbaku,msimu huu wanunuzi watafatilia sana watafumua kila mtumba ili kukagua na tukikuta umeweka uchafu tumbaku zako zitataifishwa na tukikuta umechanganya madaraja mkulima atalipa faini ya shilingi laki tano na chama cha msingi kitatozwa faini ya laki tano pia” Amesema Nyambi.

Nao baadhi ya wakulima kutoka kata ya Bulungwa na ubagwe wameishukuru bodi ya tumbaku kwa kuwapa elimu hiyo na wamekishukuru chama kikuu cha KACU kuwafikia na kuwapa maelekezo ya ufungaji wa tumbaku.
“Kwakweli sisi wakulima tunaishukuru sana bodi ya tumbaku kwa kutufikia na kutupa elimu hii sisi wakulima tulikuwa tunalima baada ya kuvuna tunaacha shamba hadi msimu ujao,Lakini pia tunashukuru sana KACU kufika na kutuelekeza ufungaji wa tumbaku naamini hakuna mkulima ambaye ataenda kinyume” Wamesema wakulima hao.