TRUMP AIPA CHINA SAA 24, YENYEWE YASEMA HAITAKUBALI

Rais wa Marekani, Donald Trump amesema ataiwekea China ushuru wa ziada wa asilimia 50 kwa bidhaa zinazoingizwa Marekani, ikiwa haitafuta ushuru wake wa kulipiza kisasi wa asilimia 34.

Trunp amefikia uamuzi huo baada ya China kuweka ongezeko hilo kama majibu kwa Trump aliyeiwekea ushuru wa asilimia 34 kwa bidhaa za China.

Trump ameipa saa 24 kufuta ushuru huo, huku China ikisema haitakubali kushinikizwa na kwamba itapambana dhidi ya nyongeza mpya ya ushuru toka Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *