TRAORÉ AKATAA NYONGEZA YA MSHAHARA, MAFISADI WAKALIA KUTI KAVU

Rais wa Burkina Faso, Ibrahim Traoré (37), amekataa kuongezwa mshahara wake na kusisitiza kuwa ataendelea kupokea mshahara aliokuwa akipata tangu akiwa mwanajeshi.

Traoré pia amewataka Maafisa wote wa Serikali kutangaza mali zao hii leo Jumatatu, Machi 24, 2025, akiongeza kuwa kutotimiza wajibu huo kutasababisha kufunguliwa mashtaka haraka.

Aidha, ameonya kuwa yeyote atakayejihusisha na ufisadi ili, kupata utajiri wa haraka ataadhibiwa, akisema hatavumilia ufisadi.

Rais Traoré pia amepiga marufuku Maafisa wote kufanya biashara na Serikali, akinadai kuwa hatua hiyo inalenga kupambana na ufisadi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *