Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imesema kupitia kongamano la wajasiriamali linawasaidia kutambua changamoto zinazolikumba kundi hilo.
TRA imesema kupitia jukwaa la kongamano la wafanyabiashara na wajasiriamali lililoandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) linalofanyika katika ukumbi wa Super Dome uliopo Masaki jijini Dar es Salaam watafahamu changamoto zinazowakabili wafanyabiashara na wajasiriamali wadogo na wa kati na kuzitafutia ufumbuzi.
Meneja Utafiti wa TRA, Saada Ally ndiye ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Aprili 27, 2023 katika kongamano hilo ambapo amesema kupitia kongamano hilo watatambua changamoto za kurasimisha biashara, usajili na kulipa kodi zinazowakabili wafanyabiashara.