TPHA YAONGEZA VITENDEA KAZI KUDHIBITI WADUDU, NDEGE WAHARIBIFU WA MAZAO

Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHA), imejipanga kuwakabili wadudu na ndege waharibifu wa mazao, baada ya kuongeza vitendea kazi, ikiwemo ndege nyuki 21 zitakazotumika katika shughuli za udhibiti wa visumbufu vya mimea.

‎Hayo yamebainishwa hii leo Agosti 27, 2026 na Mkurugenzi Mkuu wa TPHA, Prof. Joseph Ndunguru, wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa TPHA, Prof. Joseph Ndunguru.

Amesema, TPHA pia imeagiza ndege nyuki nyingine 20, ili kuongeza uwezo wa mamlaka hiyo kuyafikia maeneo mbalimbali nchini na kuchukua hatua kwa wakati dhidi ya wadudu na ndege waharibifu wa mazao.

“Kwa sasa tuna ndege 21, nyingine 20 tumeziagiza, na pia tumenunua ndege kubwa yenye uwezo mkubwa kwa ajili ya kudhibiti ndege na wadudu waharibifu wa mazao,” alibainisha Prof. Ndunguru.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *