Kwa mujibu wa Tmz Mke Wa Rapper Tory Lanez, Raina Chassagne amewasilisha ombi la talaka Mahakamani akidai kuwa sababu kuu ya kufanya hivyo ni kutokuwa kwenye maelewano mazuri na mumewe jambo linalopelekea kuwa na tofauti zisizoweza kusuluhishwa.
Katika hati zilizofikishwa Mahakamani #Raina pia ameomba haki ya malezi ya mtoto wao aitwaye Kai (7) wakati baba wa mtoto huyo akiendelea kutumikia kifungo chake cha miaka 10 jela.
Wawili hao walifunga ndoa ya siri Juni 25, 2023 kipindi ambacho #Lanez anakabiliwa na mashitaka ya kumpiga risasi aliyekuwa mpenzi wake.
Rapper huyo alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela mwezi Agosti mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kumpiga risasi nyota wa hip-hop Megan Thee Stallion.