TOKENI KIFUA MBELE, HAKUNA WA KUWATISHA OKTOBA 29 – DKT. SAMIA

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan amesisitiza hakuna kitakachotokea Oktoba 29, hivyo wananchi wanapaswa kujitokeza kifua mbele kwenda kupiga kura.

Hii ni zaidi ya mara tatu, Dkt Samia anatoa hakikisho hilo kwa Watanzania, akisisitiza vyombo vya dola na Serikali imejipanga vema kudhibiti kusudio lolote la kuathiri upigaji kura.

Dkt Samia ameeleza hayo leo, Jumamosi Oktoba 11, 2025 alipozungumza katika mkutano wake wa kampeni za urais, uliofanyika wilayani Kahama, mkoani Shinyanga.

“Nimeona Kahama wapigakura ni wengi mno, wale jamaa zetu wanaweza wakaja na vijitisho hivi ili kura zisiende kupigwa. Nataka kuwaambia tokeni kifua mbele tarehe 29, hakuna lolote litatokea, mnaowaona hapo walinzi wetu wamejipanga vizuri mno.

Hakuna litakalotokea kuko salama, tokeo kapigeni kura,” amesema Dkt Samia na kushangiliwa na maelfu ya wananchi waliofurika katika mkutano huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *