Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

TMA yatangaza Mvua kubwa Mikoa sita

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa tahadhari kwa ya uwezekano wa kunyesha mvua kubwa kuanzia leo Jumatano Novemba 22 hadi Novemba 25 ambazo huenda zikasababisha vifo kama tahadhari hazitachukuliwa.

TMA imesema mvua hizo zinatarajiwa kunyesha katika Mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Pwani, Lindi, Mtwara, Tanga na visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.

Kupitia taarifa ya Mamlaka iliyotolewa Novemba 21, 2023 katika mitandao yao ya kijamii imesema, athari zinazoweza kujitokeza ni pamoja na baadhi ya barabara kutopitika kutokana na mafuriko pamoja na vifo kwa siku hizo mbili, hivyo wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari.

Agosti 26, 2023 TMA ilitoa taarifa ya uwezekano wa kuwapo kwa mvua kubwa za El-Nino ambazo huenda zikasababisha vifo, magonjwa ya mlipuko na uharibifu wa miundombinu kuanzia Oktoba hadi Desemba 2023.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *