TMA yatabiri mvua kubwa zaidi ya mikoa 10 hadi Feb. 3

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania – TMA, imetoa muendelezo wa Utabiri wa hali ya hewa unaoonesha uwepo wa hali mbaya ya hewa kwa Siku 4, kuanzia Januari 31 hadi Februari 03 mwaka huu.

Taarifa hiyo ya mamlaka ya hali ya hewa imetoa angalizo la kutokea kwa mvua kubwa katika kipindi cha siku nne, huku ikifafanua kuwa kiwango cha athari zinazoweza kujitokeza ni za wastani.

Kulingana na utabiri huo wa TMA, hali mbaya ya hewa itakayoambatana na mvua kubwa inatazamiwa kutokea kwenye mikoa zaidi ya 10 ikiwemo Dodoma, Mbeya, Singida, Njombe, Mtwara pamoja na Morogoro.

Kufuatia hali hiyo; TMA imewataka Wananchi kwenye mikoa hiyo kuchukua tahadhari kwa Sababu mvua hizo zinaweza kusababisha Makazi kuzunguukwa na maji na kusimama kwa muda Shughuli za Kiuchumi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *