Staa muziki kutoka Nigeria, Tiwa Savage ameshatua nchini Kenya, muda huu kwaajili ya tamasha la Walker Town linalotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi katika viwanja vya Uhuru Gardens.

Katika shoo hiyo Tiwa ameahidi kutoka burudani ya nguvu kama umeme na atasindikizwa na mastaa kama Nyashinski, nguli wa Kongo, Fally Ipupa, na Dj wawili mahiri wa Afrika Kusini, TxC.
