Tiwa Savage amfungulia kesi Davido

Staa wa muziki kutoka Nigeria, Tiwa Savage, amefungua kesi polisi dhidi ya msanii mwenzake Davido.

Tiwa amefungua kesi hiyo katika  jimbo la Lagos,  siku ya Januari 9, 2024,jana ambapo amedai kuwa amekuwa akipokea vitisho vya kufanyiwa ukatili wa kimwili na Davido.

Inaelezwa kuwa mnamo Desemba 23, Tiwa alishiriki kuandika katika Instastory ya mzazi mwenzake na Davido Bi. Sophia Momodu.  Na baada ya hapo ndipo Davido alimtumia meseji meneja wa Tiwa akionyesha kuchukizwa kwake na kutumia lugha za dharau msaanii wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *