Watu tisa na wengine 2 wamejeruhiwa katika ajali mbaya iliyotokea kwenye Mteremko wa Iwambi, Mbeya Vijijini baada ya Lori aina ya Howo la #Zambia likiendeshwa na Mohamed Abilah (47) kuligonga kwa nyuma Basi dogo aina ya Mitsubish Rosa likiendeshwa na Elly Elia Mwakalindile (41)

Waliopoteza maisha ni Wanaume 5 na Wanawake 4, waliojeruhiwa ni Wanaume 13 na Wanawake 10. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema majeruhi wanatibiwa Hospitali Teule ya Ifisi ya Mbalizi na wengine wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya, miili imehifadhiwa Hospitali Teule ya Ifisi Mbalizi