TINA CHENGE AONGOZA KURA ZA VITI MAALUM SIMIYU.

Na Saada Almasi-Simiyu

Baada ya kamati kuu ya CCM Taifa kupitisha majina 8 ya wagombea nafasi ya Ubunge viti maalum mkoani Simiyu wajumbe 1034 Umoja wa Wanawake Taifa CCM wameshiriki kura za maoni na kumchagua Tinna Chenge kwa kura 631

Uchaguzi huo umefanyika katika viwanja vya Bariadi Alliance mjini Bariadi umeongozwa na mkuu wa mkoa wa Simiyu Anamringi Macha akiwa mwenyekiti wa uchaguzi huo ambaye amewataka wagombea kuwa watulivu wakati wote wa shughuli hiyo na kusema kuwa matokeo ya kura hizo yanarudishwa kamati kuu CCM Taifa.

“Hongereni kwa kazi nzuri mliyoifanya na kuwa wavumilivu katika huu mchakato lakini msifanye sherehe kupitiliza kwani haya matokeo yanarudishwa sehemu husika na huenda yakapitishwa na kamati kuu CCM Taifa hivyo niwapongeze wagombea wote na wajumbe kwa kuonyesha ukomavu wa kisiasa.

Naye katibu wa siasa na uenezi CCM mkoa wa Simiyu Lumen Mathias ameiambia Jambo Fm kuwa kuelekeauchaguzi mkuu chama hicho kimejipanga kufanya siasa za kistaarabu zisizo na machafuko kwani yapo mengi ya kusungumza katika majukwaa.

“Tumejipanga kufanya kampeni za kisayansi ili kila mwananchi apete sera za chama na kuinadi vyema ilani ya chama kwa mujibu wa ratiba itakavyotufikia ili waendelee kutuunga mkono hivyo tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi” katibu Lumen.

Kwa upande wake katibu wa wanawake CCM mkoa wa Simiyu Fatuma Ndee amewataka wanawake kujitokeza kwa wingi pale kampeni za uchaguzi zitakapoanza akiamini kuwa wanawake ni jeshi kubwa ambalo ushiriki wao ni mkubwa.

“kwa sasa kuna mwamko mkubwa sana wa wanawake kushika uongozi maana hata wenyeviti wa mitaa,madiwani wamejitokeza hiyo ni kuonyesha kuwa ile dhana ya wanawake wa kanda ya ziwa kukamdamizwa na mfumo dume sasa hivi haipo” amesema Ndee

Awali wapiga kura waliotakiwa kupiga kura ilikuwa ni 1053 japo walioshiriki ni 1034 lakini kura halali zilizopigwa ni 1029 baada ya kura 5 kuharibika ambapo wagombea wengine walioshiriki ni Grace Balele kwa kupata kura 34,Jane Masanja kura 50 ,Limi Kilalo kura 60,Rosemary Nghwani 186, Minza Simon kura 292,Karitas Machupa kura 312 na Esther Midimu aliyeshika nafasi ya pili kwa kupata kura 500

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *