Timu 12 kushiriki Mapinduzi Cup 2024

Kamati ya Kombe la Mapinduzi Cup 2024, imetangaza tarehe rasmi ya kuanza kwa Mashindano hayo, ambapo yanatarajiwa kuanza rasmi Disemba 28, mwaka huu na kukamilika Januari 13, 2024.

Akitoa taarifa mbele ya Waandishi wa Habari, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dkt. Suleiman Jabir amesema Uwanja wa Amaan ndio utakaotumika katika michuano hiyo.

Dkt. Jabir amesema kwa msimu huu, michuano hiyo itashirikisha timu 12 kutoka maeneo mbali mbali Zanzibar, Tanzania Bara na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Kwa upande wa Zanzibar, Timu hizo ni Mlandege, KVZ, Chipukizi na Jamhuri, kwa upande wa Tanzania Bara ni Simba, Yanga, Azam na Singida FG huku timu zinazotoka njee ya Tanzania ni URA (Uganda) Bandari (Kenya) Vitalo (Burundi) APR (Rwanda).

Mashindano yatachezwa kwa mfumo wa makundi na kutakuwa na Makundi matatu kila kundi litashirikisha timu nne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *