
Na Ibrahim Rojala
Fikiria umegangamala na kutafuta fedha kwa udi na uvumba,mvua ikakuyeshea baridi na joto vikawa sehemu ya utafutaji wako na baada ya hapo ukaona ni bora fedha hiyo ukaiwekeza kwenye kikundichako ulichokichagua huenda kwa miezi kadhaa au hata mwaka mzima ukiwa umeipangia malengo lukuki ya maendeleo pindi utakapoichukua lakini muda wa makabidhiano unapofika zinaanza hekaya za abunuasi mara mwenyekiti kasafiri,mweka hazina kafiwa na maelezo mengine chungu nzima.
Tigo Tanzania, kwa kutambua changamoto za aina hiyo ili kulinda kilicho chako imekuletea huduma ya Tigopesa Kikoba (Kikobadigital) ya kuweka akiba ambayo ni mfumo wa aina yake wa kuweka akiba unaoruhusu kuweka akiba kwa vikundi vya marafiki, familia au VICOBA vilivyopo.
Miongoni mwa malengo yaTigopesa Kikoba (Kikobadigital) ni pamoja na kutoa ahueni kwa Watanzania wamekuwa wakitumia njia za jadi kuweka akiba ambazo si tu kwamba si salama bali ni za usumbufu na wakati mwingine kukosa uwazi miongoni mwa waliokubaliana kutumia njia hizo ili kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza kuhusiana na huduma hii,Mkuu wa Kitengo cha huduma za kifedha na malipo Tigopesa Bw.Mshama Mshama amesema Tigo Pesa Kikoba imedhamiria kuboresha namna ya uendeshaji wa vikundi vya kifedha vya kijamii ikiwemo kuondoa changamoto ya kutokwepo kwa mifumo rahisi ya uendeshaji na udhibiti wa michango,marejesho na mikopo ya kifedha kwenye vikundi hivyo.
Ni Kwa Namna Gani Mnaweza Kujiunga na Huduma Hii?
Kusajili kikundi chenu ni rahisi, Mwenyekiti ataingia kwenye menyu ya Tigo Pesa kwa kupiga *150*01# na kuchagua namba 7, Huduma za Kifedha kisha chagua namba nane (8) Akiba ikifuatiwa na (3) Kikoba kisha utachagua 1 kusajili kikundi chenu,baada ya kusajili kikundi Mwenyekiti na viongozi wake wataongeza wanachama wengine husika kisha mnaweza kuendelea kuweka akiba kidigitali na kugawana gawio kulingana na katiba yenu.
Upekee wa Huduma Hii ni Upi?
Upekee wa hudumahii ya kipekee ni kwamba inawawezesha wateja wa mitandao mengine kuchangia pia na hivyo kuendelea kutanua Uhuru wa Kifedha miongoni mwa wanachama katika kikundi na piaTigo Pesa Kikoba ni salama na rahisi kwenye utumiaji,chaguo bora ni kujiunga na huduma ya Tigo Pesa KIKOBA uamuzi utakaowasaidia katika kuweka akiba yenu ya kesho kwasababu Tigo Pesa ni Zaidi ya Pesa Jana, Leo na Kesho.