Tigo Yakambidhi Milioni 10 Mshindi Kampeni Ya Soka La Afrika Shinyanga

Kampuni ya Mawasiliano ya simu nchini Tanzania TIGO imekabidhi zawadi ya hundi yenye thamani ya shilingi milioni kumi kwa mshindi wa Kampeni ya Afcon 2023 ya Soka la Afrika Limeitika iliyoendeshwa na kampuni hiyo ambapo Bw. Raphael Songelaeli mkazi wa Mtaa wa Mwadui Manispaa ya Shiyanga Mkoani Shinyanga ameibuka mshindi na kujinyakulia kitita hicho cha fedha.

Akizungumza wakati akikabidhi zawadi hiyo hii leo April 25,2024 nyumbani kwa mshindi,Meneja wa TIGO Mkoa wa Shinyanga Bw.Sadock Mahundo amesema kampuni hiyo imeendelea kuendesha promosheni mbalimbali kwa wateja wake na kutoa zawadi kwa washiriki wanaoibuka washindi kwa kuwafuata hadi nyumbani ili kuongeza hamasa kwa wateja wake na kuboresha promosheni hiyo na kuelezea namna mteja wa Kampuni hiyo  anavyoweza kushiriki.

“Kushiriki ni rahisi utaingia kwenye sehemu ya kuandika ujumbe mfupi utaandika neno ‘SOKA’ na kisha kutuma kwenda namba 15670 na kujibu maswali mbalimbali na hatimae kuibuka mshindi, kwa tukio hili lililofanyika leo ni ushuhuda kuwa hakuna utapeli wa aina yoyote, katika promosheni zote kutoka kampuni ya TIGO zinaendeshwa kwa kuzingatia vigezo na masharti na ni rahisi kwa yeyote kuweza kushiriki”, amesema Bw.Mahundo.

Akitoa neno la shukrani mara baada ya kupokea zawadi hiyo Bw. Raphael Songelaeli ameishukuru kamuni ya TIGO kwa kuendesha mashindano hayo na kiwasihi watu wengine kujiunga na mtandao wa TIGO ili waweze kushiriki na hatimae kuibuka washindi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *