Tiba asili ya Mafua na Kikohozi kwa mtoto

Mafua na kikohozi huleta mabadiliko katika mfumo wa kulala hasa pale mafua yanapotoka mara kwa mara, kumbatana na homa.

Asali ni dawa ya kufubaza kikohozi na mafua na tiba rahisi ambayo inaweza kutibu kikohozi na kuvimba koo. Chukua maji ya uvuguvugu. Weka nusu kijiko cha asali, tingisha mpaka ichanganyike na maji kisha mpe mtoto anywe.

Matone ya chumvi yatasaidia kusafisha njia za pua na kuondoa makamasi yaliyokwama na kuganda ambayo yanaweza kusababisha kupata shida katika kupumua. Chukua kijiko 1/4 cha chumvi na uweke kwenye kikombe kimoja cha maji, kisha koroga kupata mchanganyiko mzuri.

Tangawizi ni tiba yenye ufanisi katika kutibu kikohozi, mafua makali. Inasaidia kuongeza mzunguko wa damu na pia kuufanya mwili upate joto ili makamasi yaweze kuyeyushwa na kutolewa.

Limau ni dawa ya antibacterial na antiseptic inayoweza kutumika kutibu kikohozi na mafua. Limau pia lina kiwango kikubwa cha vitamini C ambacho husaidia katika kuimarisha kinga ya mwili. 

3 responses to “Tiba asili ya Mafua na Kikohozi kwa mtoto”

  1. Ujasema hyo matone ya maji ya chumvi anakunywa au anawekewa puani na kiasi cha maji yanayochanganywa na asali ni kiasi gani, toa maelezo yaliokamilika

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *